Jumanne , 30th Apr , 2024

Rapa Fat Joe amemtaja staa wa muziki duniani Chris Brown anafaa kuwa Tupac Shakur wa kisasa 2024 sababu yupo Original na anajua kufanya vitu vingi kwa wakati mmoja.

Picha ya Fat Joe na Chris Brown

“Bila shaka Tupac wa mwaka 2024 inabidi awe Chris Brown. Ukisema acheze Basketball naye anajua kucheza, kama kuimba anaimba kwa ubora na kurap pia anaweza tena anarap bora”

“Yupo Original ndio maana anaendelea kuwa namba 1 kwa wasanii waliosikilizwa zaidi” amesema Fat Joe

Ikumbukwe hata 50 Cent aliwahi kumpa maua yake Chris Brown kumuambia ndio mrithi wa mfalme wa muziki Pop Michael Jackson aliyefariki 2009.

Unadhani Chris Brown anastahili kuwa kama Tupac?