
Chidi Mapenzi na mke wake Shamsa Ford
Akiongea kupitia eNewz ya EATV, Chidi amesema "lile ni gari ambalo alijisikia na alilipenda akaamua kumnunulia mke wake, pesa ya kulilipia anayo lakini kinachoshindikana ni namna ya kulitoa bandarini ingawa hana wasiwasi kwa kuwa mke wake ni mvumilivu na anaishi maisha ya aina yote.
Hata hivyo Chidi amesema hataki kabisa kusikiliza maneno ya watu kwa kuwa watu wanaongea mambo mengi ikiwa ni pamoja kusema amamkimbia mke wake na kwenda China wakati ukweli ni kuwa yeye ni mtu wa kusafiri mara kwa mara kwa sababu ya biashara zake.