
Msanii wa Bongo fleva Chege chidunda
Akizungumza na Enewz Chege alisema kuwa kwa Bongo watu wanakuwa wanapoteza maadili ya dini kwasababu siku hizi miezi hii ya Ramadhani imehamia instgram kitu ambacho wengi wanakosea.
“Funga siyo kujikwida sijui manini sijui kufunga ni imani na kusali ni imani pia mwezi wa Ramadhani hauna kitu ambacho kama haujafanya hivyo haujafunga mimi nimefunga kwakuwa kinachofunga ni imani yangu na roho tusimuigizie Mungu tuwe wakweli tusifanye kwa kumuogopa fulani”, alisema Chege.