Alhamisi , 3rd Apr , 2014

Kundi kali kabisa la muziki wa Reggae hapa Tanzania, Warriors From The East wamewataka mashabiki wao kukaa tayari kwa uzinduzi mkubwa wa albam yao mpya ambayo inakwenda kwa jina Bongo Reggae, utakaofanyika hivi karibuni kwa onyesho kubwa jijini Dar.

Warriors From The East

eNewz imeongea na wasanii wa kundi hili, Black Jesus na Ras Magere kuhusiana na albam hii mpya ambayo tayari imekwishakamilika, ambapo wamesema ni kazi tofauti na yenye vionjo vya kitanzania, ikiwa na ladha mpya kabisa kwa wapenzi wa muziki wa Reggae.

Wasanii hawa pia wamewaomba mashabiki zao kuwapigia kura kuwawezesha kushinda tuzo za muziki kutoka Kilimanjaro Music Awards 2014, ambapo wameweza kuingia katika kinyang'anyiro kwa mara nyingine tena mwaka huu.