Bobi Wine
Kwa mujibu wa maafisa wa polisi, rekodi za gari hii ambayo kwa sasa ipo chini ya umiliki wa Bebe Cool zinaonyesha kuwa iliingizwa nchini na chama cha msalaba mwekundu, huku Bebe Cool akidai kuwa yeye ndiye aliyelipia gharama zake za kuingizwa Uganda, akiwa anafanya kazi na Msalaba Mwekundu kama balozi wake.
Msanii huyu amefafanua kuwa, hakuna sheria yoyote iliyovunjwa kwa yeye kumiliki gari hii, huku akidai kuwa bado anaidai Red Cross baadhi ya gharama ambazo alizilipia yeye kwa makubaliano kuwa atarudishiwa ikiwepo gari hili, baada ya kumaliza mkataba wake na chama hicho.