
Akizungumza na www.eatv.tv Bill Nass amesema endapo atapata kampuni itakayo mtambua yeye kama msanii na kumpa uhuru kuendelea kufanya mziki,basi yupo tayari kufanya kazi.
"Sitaki kuingia kwenye kampuni ya mtu nibanwe na unajua mtu yeyote anaanzisha kampuni kupata faida, kwahiyo nataka ile kazi ambayo nitafanya kila mtu apate chake na niwe free na kufanya mziki wangu na kama show itatokea kusafiri basi iwe tayari kunielewa". Amesema Bill Nass
Bill Nass amemaliza kwa kusema kuwa anaogopa kufanya kazi kwakuwa mziki una vitu vingi kama kusafiri kwahiyo hataki kubanwa na kazi na kumpelekea kuacha mziki ila endapo akipata kampuni ambayo iko tayari kuelewa anachokifanya, basi hana budi kufanya nao kazi.