Jumatatu , 18th Jan , 2016

Msanii Bebe Cool wa nchini Uganda ameshikilia msimamo wake kwa kumtetea Rais Yoweri Museveni kwa kitendo chake cha kutokuonekana katika mdahalo wa pamoja wa wagombea wote wa nafasi ya urais Uganda kunadi sera zao,

Rais Museveni katika picha na wasanii wanaomuunga mkono

Katika utetezi wake, msanii huyo ameutuhumu mdahalo huo kulenga wasomi pekee na sio wananchi wa kawaida ambao ndio wengi.

Akionekana dhahiri kuwakera wengine kwa msimamo huo, Bebe Cool ameeleza kuwa asilimia 30 tu ya wananchi wa Uganda ndio wanaoelewa vizuri Kingereza ambayo ndiyo lugha inayoendeshea mihadalo hiyo, akisisitiza kuwa Uganda bado haipo tayari kwa suala zima la midahalo inayokutanisha pamoja wagombea.

Ukiachana na hilo mambo yanaendelea kupamba moto katika suala zima ya kampeni huko nchini Uganda, zikihusisha kwa karibu wasanii ambapo sasa zimebaki siku 30 tu kufikia siku kubwa ya kupiga kura.

Tags: