Jumatatu , 5th Oct , 2015

Baraza la Sanaa Tanzania, (BASATA) kupitia afisa habari wao Aristideus Kwizera wamepongeza kipindi cha burudani cha Planet Bongo cha East Africa Radio kwa mchango wao katika kupiga muziki wa nyumbani na kuelimisha wasanii kuhusiana na sanaa yao.

Afisa habari wa Baraza la Sanaa Tanzania, (BASATA) Aristideus Kwizera

Kwizera ameeleza kuwa, BASATA imefurahishwa na namna ambavyo elimu juu ya Hakimiliki na Hakishiriki kwa wasanii imekuwa ikitolewa sambamba na burudani kali ya ngoma za kibongo kupitia kipindi hicho.