Jumanne , 3rd Nov , 2015

Star wa muziki Barnaba Classic ametoa wito kwa wasichana kujituma katika kufanya kazi mbalimbali bila kutazama jinsia kama kikwazo ama kizuizi cha kutekeleza baadhi ya majukumu.

Staa wa muziki Barnaba Classic

Barnaba amesema hayo leo kama hamasa kwa kundi hilo la vijana kupitia kampeni ya "Mimi ni Binti Thamani" kuhamasisha watoto wa kike kuwa na ari ya kijasiriamali na kukabiliana na kila kazi katika kufikia maendeleo yao.