Jumapili , 15th Aug , 2021

Klabu ya Barcelona imeripotiwa kuwafuatilia na kuangalia uwezekano wa kufanya usajili wa mshtuko kwa washambuliaji wa Arsenal Pierre-Emerick Aubameyang na Alexandre Lacazette kama Martin Braithwaite ataondoka Nou Camp kwa ada nzuri ya uhamisho.

Picha ya Pierre-Emerick Aubameyang kushoto, kulia Alexandre Lacazette

Kocha Ronald Koeman ana haha kutafuta mbadala wa kuziba nafasi ya Lionel Messi na amekiri kwamba angependa kuleta mshambuliaji mpya lakini wataweza kutimiza lengo hilo endapo tu watamuuza Martin Braithwaite kwa ada kubwa ya uahamisho.