Jumanne , 17th Sep , 2024

Rapa na mtayarishaji wa muziki Marekani Sean Combs 'Diddy' adaiwa kukamatwa na Maafisa upelelezi na Usalama (FBI) baada ya kufunguliwa mashtaka na Mahakama Kuu.

Picha ya Diddy

Diddy amekatwa katika moja ya Hotel iliyopo Manhattan jijini New York, kwa makosa mengi ya unyanyasaji wa kijinsia,kimwili na kingono na usafirishaji haramu wa binadamu.

Mwanasheria wa Diddy amesikitishwa kukamatwa kwa mteja wake na amekosoa uamuzi huo akisema #Diddy hana hatia na mashtaka yanayomkabili hayana haki yoyote.

Pia amesema Diddy ni mtu wa familia, mwenye upendo, icon ya muziki, bilionea anayejitemea na zaidi ya miaka 30 ameitumia kujenga himaya, kufanya kazi ili kuinua jamii ya watu Weusi.