Ijumaa , 20th Sep , 2024

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe, amepiga marufuku wafanyabiashara wanaonunua kahawa kwa njia ya Kangomba na kuagiza wakamatwe huku akisisitiza kuwa uwekezaji mkubwa unaofanywa katika zao hilo umelenga  kuteka soko la kahawa ya Tanzania kimataifa.

Waziri wa Kilimo Hussein Bashe

Amesisitiza kuwa serikali kwa sasa inawekeza katika kahawa kwa kugawa miche na mbolea ya ruzuku hivyo,anatarajia kupigwa vita na wafanyabiashara kutokana na kukemea kangomba lakini hatarudi nyuma kwa maslahi ya zao hilo.

Waziri Bashe amesema hayo katika muendelezo wa ziara yake Mkoani Ruvuma mara baada ya kutembelea mashamba, viwanda vya kuchakata kahawa  na skimu za umwagiliaji wilayani Mbinga na Nyasa.

"Najua haya maamuzi yatakuwa na maumivu na yatakuwa na kelele, mimi kelele nimezoea, kamateni wanaonunua kahawa kwa kangomba," amesema

Amesema, anatarajia vita kubwa dhidi ya wafanyabiashara wanaonunua kahawa kwa njia ya Kangomba na hatarudi nyuma.