Balaa la ‘Nai Nai’ ya Ommy Dimpoz 

Alhamisi , 10th Jun , 2021

Wimbo wa Ommy Dimpoz, ‘Nai Nai’ una takribani miaka 9 tangu utoke na kufanikiwa ku-set records kadhaa ikiwa ni pamoja na kumtambulisha vizuri kwenye kiwanda cha muziki wa Bongo Fleva

Picha msanii Ommy Dimpoz na Producer KGT

Na kushinda Tuzo ya KTMA kama msanii chipukizi na wimbo bora wa kushirikishana mwaka 2012 ikiwa ndio ulikuwa wimbo wake wa kwanza.

Wimbo huo aliomshirikisha Alikiba ulitokea baada ya mkongwe Dully Skyes kuwakutanisha mtayarishaji wa wimbo huo KGT na Dimpoz kipindi hicho katika studio za Dhahabu Records na kisha baadae kufanya nae kazi G Records, studio ambazo King Kiba alikuwa akifanyia kazi zake pia.

Msikilize hapa KGT akielezea.