
Bahati Simwiche
Bahati Simwiche amesema kuwa ameachia wimbo wimbo huu ili uwe baraka kwa kila atayeupata na kuusikiliza na hakika atainuliwa kiroho kila siku kiroho kupitia nguvu ya uwepo wa Roho Mtakatifu iliyopo katika wimbo huu
"Ujumbe uliopo ndani ya wimbo huu utamugusa kila mmoja katika jamii, unapoita jina la yesu lazima ukutane na muujiza wako. Pengine unapitia majaribu mengi katika maisha yako, iwe ni katika ndoa, ofisini au popote pale unapoenda kusikiliza wimbo huu utapata faraja ya kweli". Amesema Bahati Simwiche
Aidha Bahati ameongeza kuwa video ya wimbo huo itatoka hivi karibuni maana wiki ijayo ndio zoezi la kushoot video