Ijumaa , 11th Mar , 2016

Nyota wa filamu hapa nchini Elizabeth Michael a.k.a Lulu baada ya kurudi Tanzania kwa ushindi wa tuzo kutoka Nigeria, hatimaye baba yake mzazi amefunguka na kusema kuna mtu mwenye mahari ya kumposa ili amuoe mwanaye basi na aipeleke.

Baba mzazi wa msanii Elizabeth Michael.

Baba yake Lulu ameongea na E-newz na kutufahamisha bado hajapokea mahari ya mwanae na yupo tayari kupokea mahari, hivyo E-news imeamua kuutoa ujumbe huu wa baba Lulu.

Huku wengi wakidhani kuwa ujumbe huo unaweza kumfikia mtu mzima Majey ambaye kwa sasa wapo kwenye mahusiano na Lulu.

Tags: