Alhamisi , 14th Jan , 2016

AT, msanii wa muziki anayeiwakilisha Zanzibar vizuri ametoa ya moyoni kuhusiana na hali ya kisiasa inayoendelea upande huo wa Tanzania, akitaka kuundwe kwa tume kutoka Umoja wa Mataifa kusimamia uchaguzi unaotarajiwa kurudia.

Msanii wa muzki anayeiwakilisha Zanzibar, AT

AT amesema kuwa, ana wasiwasi kuwa makosa yaliyojitokeza katika uchaguzi uliopita, yanaweza kujirudia endapo tume ile ile itasimamia uchaguzi huo, kupanga tume mpya ikiwa ni suala la msingi ili kuwapatia wananchi kile wanachokitaka.