Alhamisi , 20th Feb , 2014

Msanii 2 Face Idibia ambaye anaiwakilisha vizuri bendera ya Afrika katika anga za kimataifa, yupo katika mpango wa kutua nchini Kenya kwa ajili ya kutoa burudani ya nguvu ndani ya Jiji la Nairobi.

Supastaa huyu wa Afrika ametoa taarifa hizi kupitia mtandao wa twitter bila kufafanua zaidi juu ya tarehe rasmi pamoja na tukio la ujio wake ambao tayari umeanza kusubiriwa kwa hamu kubwa.

2Face kwa sasa anafanya vizuri na remix ya kazi yake inayokwenda kwa jina Rainbow ambayo ndani yake amemshirikisha mkali wa muziki kutoka Marekani, 2Face Idibia.