
Msanii wa BongoFleva Dully Sykes
Akizungumza hayo kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio, Dully Sykes ameeleza kuwa hakuna kitu kinachoweza kumpa mtu umaarufu tofauti na kuchapa kazi.
"Kuwa tajiri au masikini ni majaliwa ya Mungu, mimi nilipata umaarufu kabla ya Facebook, WhatsApp, Instagram na Twitter, kazi ndiyo inambeba msanii ili kufikia mafanikio, hakuna mzembe anayefanikiwa hata ukitumia mitandao yote kama huna juhudi haina maana hata meneja huwa wanaangalia msanii anajitahidi vipi" amesema Dully Sykes
Aidha msanii huyo ameongeza kuwa "Kuna watu wameumbwa kusaidia watu hata wakitendwa mimi nasaidia wala sisubiri fadhila kutoka kwa mtu, nasaidia mtu nikamaliza nafanya mambo yangu na yeye afanye yake"