Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe.
Wito huo umetolewa mapema leo na aliyekuwa Waziri wa Maliasili na Utalii nchini, Mh. Lazaro Nyalandu.
Nyalandu amesema kuwa jambo la kuwaachia huru viongozi hao ambao wapo mahabusu ya Segerea jijini Dar es salaam kwa kufutiwa dhamana na Mahakama ya Kisutu, lina tija sana kwa nchi na Watanzania kwa ujumla.
Novemba 23, mwaka 2018, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu iliwafutia dhamana Mbowe pamoja na Matiko kwa madai ya kukiuka masharti ya dhamana ikiwa ni pamoja na kudharau muhimili huo.
Hata hivyo sababu zilizotolewa na Mbowe kuhusu kushindwa kuhudhuria mahakamani tarehe 8 Novemba 2018 ni kutokana na kuugua ghafla ambapo alipelekwa Afrika kusini kwa matibabu.
Inaelezwa kwamba Oktoba 28, alielekea jijini Washington DC, nchini Marekani kuhudhuria mkutano na aliporejea tarehe 31 Oktoba aliugua ghafla.
Naye Mbunge wa Tarime mjini, Esther Matiko alifutiwa dhamana kwa madai ya kukiuka masharti baada ya kushindwa kuhudhuria mahakamani kutokana na kuwepo kwenye ziara ya wabunge nchini Burundi, sababu ambayo alielezwa kwamba haikidhi matakwa ya kushindwa kufika mahakamani.
Mbowe pamoja na Matiko ni kati ya washtakiwa wa ngazi ya juu ya uongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeoleo CHADEMA ambao wanashtakiwa kwa kufanya maandamano siku moja kabla ya kufanyika uchaguzi wa jimbo la Kinondoni, maandamano yaliyopelekea kifo cha mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji, (NIT), Akwilina Akwilini baada ya kupigwa na risasi.


