Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

#AUDIO Waziri arudi darasani

Ijumaa , 18th Aug , 2017

Waziri wa Mambo ya ndani Mwigulu Nchemba ameahidi kumsomesha kijana mmoja katika shule ya msingi Ujungu huko Iramba baada ya kuonyesha uwezo wa juu katika somo la hesabu licha ya kusoma katika shule yenye changamoto nyingi ikiwepo ya miundombinu. 

Waziri Mwigulu Nchemba akiwa anafundisha

Waziri Nchemba ameshuhudia uwezo wa mwanafunzi huyo akiwa wakati alipoingia shuleni hapo na kuanza kufundisha somo la hesabu ambapo amefurahishwa na jinsi walimu wa shule hiyo walivyojitahidi kuweka juhudi zao katika kuhakikisha wanawasaidia watoto hao kutimiza malengo yao.

Waziri Nchemba akiwa kwenye ziara ndani ya jimbo la Iramba alipita shuleni hapo kusikiliza kero mbalimbali lakini pia kufuatilia hali ya taaluma ndani ya jimbo la Iramba ambapo ameshuhudia miundombinu mibovu inayohatarisha usalama kwa wanafunzi waliopo shuleni hapo na kuahidi kuirekebisha mapema iwezekanavyo.

Akiwa shuleni hapo Mh. Waziri ameahidi kujitolea kujenga nyumba za walimu pamoja na ukarabati wa vyumba vya madarasa ambavyo vinahatarisha usalama wa wanafunzi hao.

Waziri Mwigulu ametoa ahadi hiyo baada ya kutembelea shule hiyo na kusema mazingira wanayopitia waalimu pamoja na wanafunzi hao ni magumu sana ingawa walimu wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanafunzi hao wanafanya vizuri na kufikia ndoto zao.

Waziri Nchemba akimtazma mwanafunzi akikokotoa swali alilompatia

 Waziri Nchemba ameshuhudia waalimu wanaokadiriwa kuwa tisa wa shule hiyo wakiishi pamoja katika nyumba chache zilizopo shuleni hapo huku vyumba vya madarasa  navyo vikiwa si vyakuridhisha sana.

"Waalimu 9 kuishi kwenye nyumba tatu  za aina hiyo siyo jambo la kuridhisha hata kidogo na pia siyo sahihi. Pamoja na changamoto mlizonazo niwapongeze sana kwani mnafanya kazi nzuri. Katika mazingira haya magumu lakini mnatoa watoto hapa wanaenda Mzumbe ni faraja kubwa. Nina uhakika miaka 15 ijayo humu watatoka wabunge wengi kwenye shule hii," Nchemba.

"Nawaahidi madarasa na nyumba za walimu kuwa nimechukua changamoto hizi na  nitaleta 'cement' ya kiasi mnachohitaji mapema iwezekanavyo na  nitakapofika mjini nitakutana na marafiki zangu pamoja na waziri ili tuweke mikakati ya kufanya marekebisho ya shule hii pamoja na hizo nyumba" Nchema aliongeza

Waziri Mwigulu ameshuhudia ubovu wa madarasa matatu ya shule hiyo yakiwa mabovu kabisa na yenye nyufa kubwa ambayo ni hatari sana kwa usalama wa wanafunzi huku madarasa hayo yakiwa hayana sakafu kabisa.

Msikilize hapa Chini 

HABARI ZAIDI

Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa

Maandamano yetu sio kelele za wahuni - Golugwa

Nyumba ambayo mwili wa mwanaume ulikaa hadi kuharibika

Mke aishi na maiti ya mumewe akiamini atafufuka

Ofisa wa idara ya manunuzi na mikataba akimpatia maelezo mmoja wa wananchi wawaliojitokeza kutembelea banda la GGML katika maonesho ya OSHA na kujifunza namna kuzingatia usalama katika shughuli zao za kila siku.

GGML yaja na teknolojia za kisasa za uokoaji

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Rais Samia asema CDF mwanamke atapatikana 2030

Mratibu wa idara ya dharura (ERT) kutoka GGML, Mohamed Mwaimu akimuonesha mama lishe namna ya kuzima moto wakati inatopokea mtungi wa gesi unapopata hitilafu na kulipuka. Mafunzo hayo yametolewana GGML kwa kushirikiana na OSHA kwa akina mama lishe 50 wa mkoani Arusha.

Mama lishe wafundishwa kulikabili janga la moto

Picha ya AY kulia na Mr II Sugu kushoto

AY Starring wa muziki wa BongoFlava