Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la hisa, DSE, Moremi Marwa
Akizungumza na waandishi wa habari, leo jijini Dar es salaam, Afisa Mtendaji Mkuu wa Soko la hisa, DSE, Moremi Marwa amesema uwekezaji wa ndani umechangia utendaji mzuri katika soko, ambapo uwekezaji katika hisa kwa mwaka 2020 ni bil. 591 ambapo ni pungufu ya bil. 33 ukilinganisha na mwaka 2019 huku uwekezaji katika hati fungani ukiwa mara mbili ya uwekezaji wa mwaka 2019.
“Kwa mwaka 2020 utendaji wa soko wa maeneo mbalimbali umekuwa ni mzuri ukilinganisha na mwaka 2019, mwaka 2020 kulikuwa na changamoto kwa upande wa uwekezaji hususani wawekezaji kutoka nje kupungua, lakini wawekezaji wa ndani wamechangia sana uwekezaji wa ndani uwe mzuri” amesema Moremi Marwa
ameongeza kuwa “Kwa upande wa uwekezaji hisa katika soko ulikuwa bil. 591 japokuwa ni pungufu kwa takribani bil. 33 ukilinganisha na mwaka 2019 lakini bado ni kiwango kizuri ukilinganisha na wastani, kwa wastani ndani ya kipindi cha miaka mitano uwekezaji katika soko la hisa na miamala inayofanyika ni bil. 553 kwa mwaka jana ili niongezeko ukilinganisha na wastani wa 2020”
Aidha Afisa Mtendaji Mkuu wa DSE amesema mwaka 2021 wataendelea na utekelezaji wa mkakati waliouanzisha wa soko la hisa wa kuhamasisha uwekezaji wa soko ili kuwa sehemu ya ukuwaji wa uchumi huku akisiistiza kuwa bado elimu na uelewa wa watanzania kuhusiana na soko la hisa bado ni changomoto .