Ijumaa , 30th Apr , 2021

Wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa CCM wamemchagua Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho kwa kura za ndiyo 1862 sawa na asilimia 100 ya kura zote

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mhe. Samia Suluhu Hassan

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo Mwenyekiti wa Uchaguzi ambaye ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai amesema hakuna kura ya hapana.

''Jumla ya kura zilizopigwa ni 1876, hakuna kura iliyoharibika na hakuna kura hata moja ya hapana, hivyo ameshinda kwa asilimia 100,'' amesema Mhe. Job Ndugai