
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipata chanjo ya #UVIKO_19 baaada uzinduzi wa zoezi la uchomaji wa Chanjo, Ikulu Jijini Dar es Salaam leo tarehe 28 Julai, 2021.
Dkt. Gwajima amesema hayo leo katika uzinduzi wa chanjo ya corona uliofanyika Ikulu, Jijini Dar es Salaam, ambapo amesema wamedhamiria kupeleka ufafanuzi kwa wananchi mpaka mlangoni kwa kutumia teknolojia au mtandao wa wataalum ili wananchi waweze kuamua kwa usahihi kuhusiana na suala la kuchanjwa.
“Elimu itawafanya wananchi wajue chanjo ya Johnson & Johnson ambayo tumeipokea Tanzania, imeshatolewa kwa wananchi zaidi ya milioni nane Marekani na pia kwa nchi nyingine duniani, na hizi taarifa kwamba imesitishwa ni uongo, ni kawaida kwenye mnyororo wa ugavi, shehene zinapotembea ikifika mahali ukaona hata wamesahu label lazima usitishe hurudi ukajiridhidhe, walifanya hivyo tarehe 11/04/2021, tarehe 23 Aprili wakaclear chanjo zikaendelea kutolewa na ndio tumezipokea,” amesema Waziri Dkt. Gwajima.
Pia Dkt. Gwajima amesema kuwa wamejiandaa kujibu kisayansi, kwa ushahidi na hekima hoja zote zinazotokea kwenye mtandao na nyingine ambazo zitajitokeza hapo baade.
Aidha, Waziri Gwajima, amesema Serikali inatarajia kuingiza aina tano za chanjo ya ugonjwa wa Corona ili kila mwananchi apatiwe inayoendana na afya yake. Nna Chanjo hizo ni Moderna, Pfizer-BioNtech, Johnson &Johnson, Sinopharm na Sinovac.