
Pichani, Nahodha wa Taifa Stars anayecheza Klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta, Kulia ni mwanamitindo wa kimataifa, Flaviana Matata
Waziri Kigwangalla amesema kwamba wakati huu wapo kwenye kuandaa mkakati mahsusi, kwa ajili ya kujitangaza kwenye nchi hiyo.
"Tayari pia tumeanza mazungumzo na mcheza soka wa kulipwa, Ndg. Mbwana Samatta, ili tutumie jina lake kufungua soko jipya la Utalii nchini Belgium. Tunaandaa mkakati mahsusi kwa ajili ya kujitangaza kwenye nchi hii,"
amesema Waziri.
Mbali na kuweka mipango juu ya Samatta, Waziri huyo amemuomba Mwanamitindo wa kimataifa, Flaviana Matata kukubali uteuzi wake wa kuwa Balozi wa hiari wa Utalii nchini.
"Tunakushukuru na kukupongeza Ndg. Flaviana Matata kwa uzalendo wako. Tutakupa hati ya shukrani na pia tunakupa Safari ya siku 5 kwenye maeneo ya vivutio siku yoyote utakayokuwa tayari. Pia tutaomba ukubali uteuzi wangu wa kuwa Balozi wa hiari wa utalii" Waziri Kigwangalla.
Pamoja na hayo Waziri amesema kwamba tayari amekwisha kamilisha kazi ya kubuni kauli mbiu ya #TanzaniaUnforgettable ambayo itaitambulisha nchi kwenye masoko ya utalii.