Waziri Mkuu akiongoza wabunge kuaga mwili wa Marehemu Hafidh Tahir Ali
Bw. Tahir amefariki saa 9 alfajiri ya kuamkia leo katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma na mwili wake kuagwa katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma kabla ya kusafirishwa kwenda Zanzibar kwa mazishi.
Akizungumza katika tukio hilo, Waziri Mkuu ametoa pole kwa Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai, familia ya marehemu na wabunge wote.
“Tumepokea taarifa za msiba huu kwa mshtuko mkubwa. Leo tupo katika wakati mgumu sana. Tumeondokewa na viongozi wengi,” amesema.
Spika wa Bunge, Job Ndugai akiaga mwili wa Hafidh Ali Tahir
Amesema wafiwa wanatakiwa kuishi kwa upendo. “Tumuombee marehemu, tuiombee familia iwe na moyo wa utulivu katika kipindi kigumu cha kuondokewa na mpendwa wao.”
Bw. Hafidh alizaliwa Oktoba 30, 1953 na aliwahi kuwa Mkuu wa Sauti ya Tanzania Zanzibar (1970-1978) na amekuwa mbunge tangu 2005 hadi mauti yanamkuta
Marehemu Hafidh Tahir Ali, enzi za uhai wake
Enzi ya uhai wake, alishiriki kikamilifu katika masuala ya michezo; alikuwa mwamuzi wa soka mwenye beji ya FIFA na kocha msaidiizi wa timu ya soka ya Bunge.
Hadi jana, Bw. Hafidh alishiriki katika shughuli mbalimbali ikiwemo uchaguzi wa kupata viongozi wa Tawi la Umoja wa Wabunge WanaYanga mjini Dodoma ambapo yeye alichaguliwa kuwa Katibu.
Wabunge wakiwa wamesimama kimya kwa dakika moja bungeni kuomboleza kifo cha mhe. Hafidh Ali Tahir