Waziri wa ujenzi uchukuzi na mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amewabadilishia maeneo ya kazi watumishi 3 wa mamlaka ya bandari nchini TPA kwa kushindwa kuendana na kasi ambayo wizara inaitaka kwenda nayo.
Amebainisha hayo hii leo wakati alipokuwa anaongea na waandishi wa habari na kuwataja watumishi hao kuwani pamoja na Peter Gawilo aliyekuwa afisa rasilimali watu, Mashaka Kashanga aliyekuwa kaimu mkurugenzi wa manunuzi na Kilian Charles aliyekuwa kaimu mkurugenzi wa TEHAMA.
Aidha ameifungia kampuni ya simu ya kimataifa ya Six Telecom kwa kosa la kukwepa kulipa kodi na kwa kutolipia leseni kwa wakati hali iliyoisababishia serikali hasara kubwa na kuahidi hapo kesho kuzifungia Radio 28 nchini ambazo zimeshindwa kulipia leseni za kufanya kazi nchini.




