Jumanne , 8th Jul , 2014

Naibu Waziri Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Mhe.

Naibu Waziri Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Mhe. Pindi Chana.

Naibu Waziri Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Mhe. Pindi Chana amewataka watumishi wa umma kubadilika kiutendaji kutokana na mabadilio ya Sayansi na Teknolojia na kuacha kufanya kazi kwa mazoea.

Ameyasema hayo mjini Dodoma wakati wa uzinduzi wa baraza kuu la tatu la wafanyakazi. Kwa niaba ya Celina Kombani, Chana amesema kuwa watumishi wa Umma wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya kuwapo kwa kukua kwa tekinolojia ambapo watu wengi wanao watumikia wanazijua sheria.

Nao baadhi ya wajumbe wabaraza hilo, Rais wa Chama Cha Walimu Tanzania (CWT) Gratian Mukoba, Katibu Tawala Mkoa wa Mbeya, Marry Mtunguja pamoja na Katibu tawala Mkoa wa Lindi Abdalah Chonda wamesema kuwa kazi yao itakuwa kuishauri Serikali kukabiliana na changamoto mbalimbali na kuhakakisha baraza linafanya kazi yake kwa usahihi.

Wakati huo huo, Tume ya taifa ya Kudhibiti Ukimwi nchini Tanzania TACAIDS, imesema kumekuwa na mwamko mkubwa wa wananchi kujitokea kupima virus vya ukimwi kwa hiari hali inayotokana na elimu ya kujitambua kuwafikia wananchi kwa kiwango kikubwa.

Akiongea jijini Dar es salaam hapo jana, Afisa Uraghibishi wa TACAIDS, Saimon Keraryo amesema zaidi ya watu 1,000 wengi wao wakiwa ni wanaume wamejitokeza kupima virusi vya ukimwi katika siku sita za maonesho ya biashara ya sabasaba barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam

Keraryo amesema maonesho hayo Yamekuwa ya mafanikio kwa kuwa yameinua ari ya watanzania kupima afya zao ili kujua kama wana maambukizi ya virus vya ukimwi ama la.