Jumanne , 9th Feb , 2016

Watendaji wakuu serikalini wametakiwa kutekeleza wajibu wao kulingana na dira ya taifa inavyoelekeza ili lengo la nchi kuwa na uchumi wa kati wa viwanda liweze kutimia ikiwa pamoja na kuhakikisha kuwa uslama wa nchi unaendelea kulindwa.

Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue akisisitiza jambo katika mkutano na waandishi wa habari

Agizo hilo limetolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue mara baada ya kufngua mafunzo ya usalama wa nchi kwa makatibu wa wakuu na manaibu katibu wakuu wa wizara pamoja na makatibu Tawala wa mikoa na baadhi ya viongozi wa Majeshi.

Balozi ombeni sifue amesema kuwa mafunzo hayo yatawaelimisha viongozi hao kuelewa maslahi ya nchi ya ndani na kimataifa ikiwa ni pamoja na kufanya maamuzi kwa upeo mpana wa kujali maslahi na Usalama wa Taifa.

Watu mbalimbali wanatarajia kutoa mada katika mafunzo hayo ya wiki moja ambayo yanawalenga zaidi watendaji wakuu wa serikali, akiwemo waziri Mkuu mstaafu Salim Ahmed Salim.