
Kebwe Stephen Kebwe - Mkuu wa Mkoa wa Morogoro
Hayo yalisemwa jana Mkoani Morogoro na Mkuu wa mkoa wa huo Dkt. Kebwe Stephen Kebwe wakati akifungua mkutano wa madaktari wa afya ya kinywa na meno wanaokutana ambapo amesema magonjwa yasiyoambukiza yakiwemo ya kinywa na meno yameendelea kushika kasi kutokana na watu kusahau kupima afya zao.
Naye Rais wa chama cha madaktari wa afya ya kinywa na meno anayeandaliwa, Dkt. Ambege Mwakatobe, akabainisha wamekusudia kuboresha huduma ili kwenda sambamba na ukuaji wa uchumi.
Dkt. Lorna Carneiro
Kwa upande wake Rais wa chama cha madaktari wa afya ya kinywa na meno Tanzania (TDA) Dkt. Lorna Carneiro, pamoja na kuwahimiza watanzania kupiga mswaki mara mbili kwa siku kwa kutumia dawa ya meno yenye madini ya Floride yanayosaidia kuua vijidudu mdomoni na kubadilisha mswaki, ameitaka serikali kukutana na wadau na kuangalia namna bora ya kutoa misamaha ya kodi kwenye vifaa tiba.