Jumamosi , 26th Apr , 2014

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo amewaongoza Watanzania katika maadhimisho ya miaka 50 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar, katika sherehe zilizofanyika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Mmoja kati ya askari wa Miamvuli akishuka toka angani umbali wa futi 4500 toka usawa wa bahari

Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo amewaongoza watanzania katika maadhimisho ya miaka 50 ya muungano wa Tanganyika wa Zanzibar uliofanyika Tarehe 26 April 1964 na kuunda Tanzania.

Dkt Kikwete ameongoza maadhimisho hayo hayo katika sherehe kubwa zilizofanyika katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam ambapo maelfu ya watanzania wamejitokeza na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.

Katika sherehe hizo ambazo zimevutia hisia za wengi, kumefanyika maonesho mbalimbali ikiwa ni pamoja na Gwaride la ukakamavu kutoka kwa majeshi ya ulinzi na usalama kwa Amiri Jeshi mkuu ambaye ni Rais Kikwete.

Mengine ni maonesho mbalimbali ya zana za kivita ikiwa ni pamoja na vifaa vya ulinzi na usalama, ndege za kivita, magari ya kivita, na vifaa vya ulinzi wa majini na nchi kavu nakadharika.

Maonesho mengine ni pamoja na ushupavu wa kuruka kutoka angani ambapo askari wa mianvuli wameonesha uwezo wao kwa kuruka kutoka angani takriban futi 4500 kutoka usawa wa bahari pamoja na makomandoo ambao wameonesha ukakamavu pamoja na uwezo wa majeshi yetu kupigana bila kutumia silaha ambapo wameweza kuvunja vitu mbalimbali ikwa ni pamoja matofari na fimbo ngumu kwa kutumia viungo vya miili yao.

Maonesho mengine ni pamoja na onesho la mbwa aliyefunzwa na maonesho ya kuzuia vurugu magerezani

Vijana wa halaiki pia hwakuwa nyuma kwa kutoa ujumbe mbalimbali wa muungano kwa njia ya kuchora maumbo mbalimbali.

Kauli mbiu ya miaka 50 ya Muungano ni 'Utanzania wetu ni Muungano Wetu, Tuulinde, Tuuimarishe na Kuudumisha'.