Chalamila ametoa kauli hiyo mkoani Mbeya, ambapo amesema njia ya kutumia bakora ni miongoni mwa njia ambazo zinasaidia sana kwenye kuhamasisha jambo.
"Siku hizi tunatumia bakora katika kila jambo, tukikukuta umekaa nyumbani na huolewi ni bakora tu nenda katafute mume na ukiwa umekaa nyumbani huoi ni bakora tu nenda katafute mke, kuna umri ambao unatosha lazima uchangamshwe'' amesema Chalamila.
Hivi karibuni Mkuu wa Mkoa huo, alitawala kwenye vyombo mbalimbali vya habari baada ya kuonekana anawachapa bakora baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari Kiwanja, iliyopo Chunya mkoani Mbeya, baada ya kuteketeza kwa moto mabweni yao.