Kila kiungo cha Ng’ombe kina thamani kauli hii inadhihilika baada ya Raphael Farijara muuza Damu wa eneo la machinjio ya Vingunguti ambapo anatueleza namna Damu hiyo inavyoenda kuwa bidhaa.
“Hii ni Damu ya Ng’ombe ambayo inaokotwa machinjioni ikija hapa tunaipika tukishaipika tunaikausha ndani ya siku mbili au tatu inakuwa imekuwa tayari kwa kuuzwa, Damu hizi zipo aina mbili ya Ng’ombe na Mbuzi kwahiyo na bei yake ni tofauti ya Ng’ombe Iko juu kwa sababu ni nzito na ya Mbuzi ni nyepesi kwahiyo bei yake inakuwa chini kidogo”, Raphael Farijara Mpishi wa Damu.
Kila kazi ina changamoto zake kazi hii Ina changamoto gani?
“Zamani tulikuwa tunafanya biashara ndani ya ukuta wa machinjio lakini pameuzwa kwahiyo tumeletwa nje, hapa tulipo ni padogo tupo watu Kama 50 kwahiyo hapatoshi utakuta Damu Ina siku tatu na haijakauka kwa sababu eneo ni finyu sana”, Raphael Farijara -Mpishi wa Damu.
Vijana wanapewa ushauri gani kuhusu ukosefu wa ajira?
“Nashauri vijana wenzangu waache kuchagua kazi kwa maana riziki ya mtu ipo mikononi mwa mtu kikubwa tujitume”, Athanas Faustine -Mkazi wa Vingunguti
“Serikali ituboreshee miundombinu ili vijana waweze kujiajiri inapotokea wamekosa ajira”, Lameck Mchiwa -Mkazi wa Vingunguti.
“Tukiwezeshwa tunaweza sio kila mtu amesoma sio kila mtu anaweza kazi za ofisini lakini mazingira yakiwa rafiki hakuna anayeweza kulia kuhusu ajira watupunguzie masharti ya mikopo ili tuweze kujiairi “, Joseph Masala-Mkazi wa Vingunguti.