Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Ramadhani Mungi.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la polisi mkoani ACP Prudensiana Protas amesema ajali hiyo imetokea katika barabara kuu ya Iringa kwenda Mbeya.
ACP Prudensiana amesema watu wawili wamejeruhiwa katika ajali hiyo na wanaendelea kutibiwa katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa na hali zao zinaendelea vizuri.
Katika tukio la pili Kaimu Kamanda amesema watu wawili wamefariki baada ya pikipiki mbili kugongana uso kwa uso katika eneo la Mgela-Kiwere barabara ya Iringa-Pawaga wilaya ya Iringa Vijijini.
Hata hivyo, Kaimu Kamanda wa polisi mkoani Iringa ACP Prudensiana Protas amewataka wananchi kudumisha amani katika kipindi cha sikuku ya Iddi.