Jumanne , 17th Mei , 2022

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema serikali ya awamu ya Sita inaendelea kukamilisha miradi yote ya maendeleo iliyoanza wakati wa serikali ya awamu tano huku akisisitiza kuwa miradi mingi imeanza kukamilika.

Rais Samia amesema hayo Mkoani Tabora wakati wa uzinduzi wa barabara ya Nyahua  - Chaya Mkoani Tabora yenye urefu wa KM 85.4  ambapo amesisitiza kuwa Serikali ya awamu ya sita inaendelea kukamilisha miradi ya maendeleo iliyoanza katika serikali ya awamu ya tano ambapo amesema wanaosema serikali yake imeiacha baadhi ya miradi ni uongo 

Aidha Rais Samia amewataka wananchi kuhakikisha wanatunza miundombinu inayojengwa na serikali ikiwemo barabara na madaraja ili iweze kudumu na kuchangia katika maendeleo 

Katika hatua nyingine Rais Samia amewaagiza mawaziri kufanya ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za UVIKO - 19 zinazotumika kukamilisha miradi mbalimbali ya maendeleo huku akisema mwisho wa matumizi ya fedha hizo ni mwezi ujao (June) mwaka huu, ambapo amemuagiza Waziri wa Tamisemi kuhakikisha anasimamia tenda zote kukamilika kwa wakati