Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid.
Kauli hiyo imetolewa na kamishna msaidizi kutoka wizara ya afya na ustawi wa jamii kitengo cha haki za mtoto na marekebisho ya tabia, Stephen Gumbo kwenye mkutano mkuu wa shirika lisilo la kiserikali la kulea watoto la Kisedet mjini Dodoma.
Gumbo amesema kuwa kwa kipindi kirefu sasa serikali haijafunga vituo vya kulelea watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani kutokana na kutokidhi vigezo lakini kuna baadhi ya vituo ni lazima vifungwe kutokana na kutokidhi vigezo.
Aidha amewataka watanzania kuwalinda na kutoa taarifa za mauaji ya watoto wenye ualbino kwani mauaji ya watu wenye ualbino nchini yanalitia doa taifa katika anga za kimataifa.
Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa shirika la kisedet, Jacob Mhepe amesema kuwa wamekuwa wakikabiliwa na changamoto nyingi katika kuwalea watoto wanaoishi na kufanya kazi mitaani kutokana na jamii kutokuwa na mwamko wa kuwasaidia watoto hao.