Ijumaa , 3rd Jul , 2015

Wananchi mkoni Njombe wametakiwa kuchagua viongozi waadilifu ifikapo Oktoba 25 mwaka huu ili waweze kupata uwakilishi mzuri badala ya kuwapa nyadhifa watu wanaotaka kujinufaisha wenyewe.

Baadhi ya viongozi wa Chama cha Demokrasia Mkoani Njombe wakiwa kwenye msafar wa kumsindikiza mtia nia wa kugombea ubunge Njombe Kusini.

Hayo yamebainishwa katika jimbo la Njombe kusini linalotawaliwa na spika wa bunge la Tanzania Anna Makinda linaonekana kupata upinzani mkubwa kufuatia idadi ya wagombea kuendelea kujitokeza kutangaza nia ya kutaka kuliongoza.

Akitangaza nia mgombea wa nne kutangaza nia ya kuwania ubunge wa jimbo la Njombe Kusini, Rafaeli Rulandala ambaye ni mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema mkoa wa Njombe katika mkutano wa hadhara na kufanya idadi ya wanao wania kugombea kwa tiketi ya chama hicho kufikia 11 huku chama cha Mapinduzi wakifikia 4.

Rulandala amesema pamoja na idadi kubwa ya wanaowania kuteuliwa kuwania nafasi hiyo atakuwa tayari kumpa ushirikiano atakaye teuliwa kuipeperusha bendera ya kwa tiketi ya CHADEMA ili kuhakikisha jimbo hilo linachukuliwa kutoka chama tawala

Ameeleza kuwa jamii kwa sasa inakabiliwa na changamoto nyingi katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu, kilimo na miundombinu ambapo kama atateuliwa atavipa kipaombele.

Aidha Lulandala amesindikizwa na katibu wa chama hicho mkoa wa Njombe ambaye pia ni mtangaza nia, Alatanga Nyagawa alionesha masikitiko yake dhidi ya dhuluma kwa wananchi inayofanyika na vingozi wa chama hicho akitolea mfano ubadhirifu katika halmashauri ya wilaya ya Njombe na hospitali ya wilaya ya Njombe

Mkutano huo wa kutangaza nia umehudhuriwa na mtangazania kutoka jimbo la Njombe kaskazini Oraph Mhema ambaye ni msemaji wa jumuiya ya wafanyabiashara mkoa wa Njombe na mjumbe wa halmashauri kuu Chadema mkoa wa Mbeya Joseph kasambala

Kasambala alisema kuwa wananchi wakubali kuwa mabadiliko hayatakuja kama wataendelea kuchagua viongozi kama Anna Makinda hakutatokea uongozi wa chama kingine.