Ijumaa , 19th Jul , 2024

Wananchi na Wanachama wa SACCOS Ya Lupembe Iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Wametaka Kurudisha Kwa Fedha Katika Saccos Hiyo zaidi ya Shilingi Milioni 600 zinazo Daiwa Kutafunwa na Viongozi wa saccos hiyo.

Awali Baadhi ya wananchi na wanachama wa Lupembe Saccos Wanasema wamekosa imani na bodi pamoja na ushirika na hivyo wanataka fedha zao Ili Wakafanyie shughuli zao.

Kutokana na Hali Hiyo Mkuu wa wilaya YA Njombe Kissa Kasongwa ameagiza kukamatwa kwa wajumbe wote wa bodi ya Lupembe Saccos ndani ya saa 48 ili warejeshe fedha hizo huku akielekeza kukamatwa na kuhojiwa kwa Ofisa ushirika wa halmashauri ya wilaya ya Njombe Fredy Mwankusye ambaye anatajwa kushindwa kusimamia vyama vya ushirika .

Edwinswalle ni Mbunge wa jimbo la Lupembe ametaka viongozi wote waliosimamishwa kazi wakamatwe na waanze kuhojiwa ili fedha za wananchi wa Lupembe zirejeshwe huku Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Njombe akisema lazima fedha za wananchi zirejeshwe.

Awali meneja wa Lupembe Saccos Oliver Kinyamagoha aliyesimamishwa kazi amesema kutokana na changamoto kubwa iliyojitokeza anaomba msaada wa kufanyika kwa uchunguzi.