
Wamesema mvua zilizonyesha zimesababisha barabara nyingi kuharibika kutokana na kujengwa chini ya kiwango na hivyo zisipokarabatiwa zinaweza kusababisha ajali za mara kwa mara hasa nyakati za usiku kutokana na kumeguka pembeni na kuzifanya kuwa nyembamba.
Wakazi hao Bw. Salum Mponda mkazi wa Kijitonyama na Bw. Leonard Tarimo ambaye pia ni mkazi wa Kijitonyama wamesema ujenzi wa barabara usiozingatia viwango, ndio sababu kubwa ya barabara nyingi kuharibika hasa nyakati za mvua.