Jumanne , 28th Apr , 2015

Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na kupamba na rushwa nchini (TAKUKURU) mkoa wa Dodoma, Emma Kuhanga amesema kuwa wananchi wamekata tamaa na serikali jinsi inavyoshughulikia watu wanaokula rushwa kubwa hapa nchini.

Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na kupamba na rushwa nchini (Takukuru) mkoa wa Dodoma, Emma Kuhanga.

Kuhanga ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Dodoma.

Amesema wananchi wamekuwa wakisikia watu wanaodaiwa kula rushwa kubwa hapa nchini lakini kitu cha ajabu ni namna serikali inavyoshughulikia watu hao na kuona kama serikali haijadhamiria kupambana na rushwa nchini.

Amesema hali hiyo imewasababisha wananchi wengi ambao ndiyo mashahidi muhimu katika kesi za rushwa kutokutoa ushirikiano pindi kesi zinapopelekwa mahakamani hali ambayo husababisha hata baadhi ya kesi kutokupelekwa mahakamani kabisa.

Mwanaidi Mrisho mkazi wa Dodoma amesema wakati mwingine huwa wanalazimika kutoa fedha ili waweze kupata huduma wanazozitaka kwani bila kufanya hivyo watoa huduma huwa hawawasikilizi.