Jumapili , 25th Aug , 2024

Watoto Sita ambao ni wanafunzi wa shule ya Msingi Ochuna wilayani Rorya wamefariki Dunia wakiwa wanaongelea katika bwawa la skimu ya umwagiliaji.

Imeelezwa kuwa chanzo cha kifo cha watoto hao ni kuzama katika tope ambalo lipo ndani ya bwawa hilo ambapo awali watoto hao walikuwa Saba, sita ndio waliingia kuogelea mmoja akabakia baada ya kuona wenzake wameshindwa kutoka katika bwawa hilo alienda nyumbani kuwa taarifu wazazi.

Mkuu wa Wilaya ya Rorya Juma Chikoma amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema watoto hao walizama jana Agosti 24 majira ya jioni ila mpaka sasa miili ya watoto hao imeshaopolewa kutoka katika bwawa hilo.