Jumatano , 23rd Nov , 2022

Mzee John Sanga(81) mkazi wa Mtaa wa Power House mjini Njombe na Mkewe Mariam Sanga(62)wamesema maisha yao yako hatarini kutokana na vitisho wanavyopokea kutoka kwa mtoto wao ambaye anashinikiza familia hiyo kugawa mali anazodai zilichumwa na mama yake kabla hajatengana na baba yake.

Nyumba yenye mgogoro

Kwa mujibu wa Mzee huyo anasema hana kikwazo kwenye uamuzi wa mahakama wa kugawana mali walizochuma pamoja na mke wa kwanza kabla ya kutengana 1977 kwasababu ya kukosekana kwa maelewano, lakini kinachomteza ni vitisho vya mwanae Matson Sanga ambaye ameorodhesha mali zilizochumwa na mke wasasa ikiwemo nyumba anayoishi sasa.

Wakieleza mwenendo wa sakata hilo lililodumu kwa kwa miaka 22 linavyoathiri maisha yao Mzee Sanga na Mkewe wa sasa wanasema wao wameridhia uamuzi wa kugawana mali zilizochumwa kabla ya 1977 lakini kitendo kinachofanywa na kijana aliyelelewa na mama mdogo tangu akiwa na umri wa miaka mitatu cha kutishia kuwafirishi mali ndiyo kinatishia usalama wa maisha yao na kwamba wanaziomba mamlaka kuwasaidia katika kipindi wakisubiri hukumu.

Kutokana na Kuhofia usalama wao wazee hawa wakalazimika kuitumia fursa uwepo wa wiki ya usaidizi wa kisheria mkoani Njombe iliyofanywa na kituo cha sheria na haki za binadamu nchini LHRC kuomba ushauri kwa mawakili juu ya mkasa unaoikabili familia yao ,na hapa Mkurugenzi wa Uchechemuzi na maboresho wa taasisi hiyo Fulgance Massawe anaeleza.

Kufuatia wazee hawa kudai kutishiwa na mgogoro wao kuchochewa mtoto mmoja wa aliyekuwa mke wa Sanga ,kituo hiki kikamtafuta bwana Matson Sanga kwa njia ya simu na hii ndiyo ilikuwa kauli yake.

Wakati wasaidizi wa kisheria wakiguswa na kuanza kumsaidia mzee huyu ili mali alizochuma baada ya kutengana na mke wa kwanza zisigawanywe ,siku chache zilizopita Mkuu wa mkoa wa Njombe Anthony Mtaka alionya watoto wenye kiu ya kupoka mali za wazazi wangali hai.

Katika ripoti iliyotolewa na LHRC baada ya kutumia siku 10 kutoa usaidizi wa kisheria mkoani Njombe imeonyesha mkoa huo unakabiliwa na changamoto kubwa ya migogoro ya ardhi ikifuatiwa na Mirathi na ndoa.