Akizungumza kwa njia ya simu katika maadhimisho ya Siku ya Waalimu Duniani, yaliyofanyika Kimkoa katika jiji la Arusha Rais Dkt. Samia ameeleza kuwa serikali inatambua mchango mkubwa wa waalimu nchini.
Pia, katika sherehe hizo, serikali kwa ushirikiano na wadau ikiwemo benki ya exim, iliunga mkono mkakati uliozinduliwa na Rais samia wa matumizi ya nishati safi ya kupikia kwa kugawa majiko ya gesi kwa waalimu zaidi ya elfu nne.
Waalimu walieleza jinsi majiko hayo ya gesi yanavyorahisisha shughuli zao za kila siku na kupunguza uharibifu wa mazingira.