Jumamosi , 2nd Jul , 2016

Wakuu wa wilaya wapya mkoani Mtwara wameahidi kufanya kazi kwa kujituma na kuwatumikia wananchi wao ili kuendana na kasi na sera ya Rais wa Tanzania Dokta John Magufuli, ambayo imejikita katika kujali masilahi ya wananchi wa hali ya chini.

Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego.

Wameeleza hayo mkoani humo mara baada ya kumalizika kwa zoezi la kuapishwa lililofanywa na mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego, na kuongeza kuwa kitendo cha kuteuliwa kwao ni kutokana na kuaminiwa na Rais, hivyo na wao lazima wajenge Imani kwa wananchi.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego, amewashukuru wakuu wa wilaya waliopita kwa kushirikiana vizuri kiutendaji na kuwataka wakuu wapya kufanya kazi kwa kujituma pamoja na kukubali kuwa ni watumishi wa wananchi.

Wakuu wa wilaya watano wa wilaya zote mkoani humo wameapishwa kiapo cha utii kazini tayari kwa kuanza kutekeleza majuku yao.

Sauti ya Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego,