Alhamisi , 23rd Jun , 2016

Karibu wakimbizi 200 waliokimbia wapiganaji wa kundi la Boko Haram wamekufa kwa njaa katika mwezi uliopita huko Bama, Nigeria kwa mujibu wa shirika la kujitolea la MSF.

Hali hiyo inayohitaji msaada wa kibinadamu wa haraka, imebainika kutokea kwenye kambi ya wamkibizi iliyotembelewa na MSF yenye watu 24,000.

Wengi wao wapo katika hali duni na kuchanganyikiwa, pia mtoto mmoja kati ya watano anaugua utapiamlo mkali, shirika la MSF limesema.