Jumanne , 3rd Aug , 2021

Wakili Shehzad Walli ameeleza alivyosota gerezani Keko kwa miezi 14 pasipokuwa na kosa huku akibainisha kuwa chanzo cha tukio hilo kuwa hamisho la fedha lililoingizwa kwenye akaunti yake ya benki.

Wakili, Muanzilishi na Mkurugenzi wa Utu Kwanza Shehzad Walli (Kushoto)

Akizungumza na kipindi cha Supa Breakfast Muanzilishi na Mkurugenzi wa Utu Kwanza Wakili Shehzad ameeleza kuwa kisa chake hicho ndicho kilimfanya ahamasike kuwasaidia wasio na makosa gerezani kupitia taasisi yake ya Utu Kwanza.

“Nilikaa gerezani miezi 14, kilichonipeleka ni transaction ya benki iliyopitishwa katika akaunti yangu na meneja kuna nyaraka ziliwekwa kwangu kwa sheria, uchunguzi ikagundulika si hivyo bali ziliwekwa na kutolea, Kesi ilianzishwa wakati najiandaa kwa ajili ya kwenda kufanya mahojiano kama shahidi bahati mbaya kufika pale nikaambiwa wewe mtuhumiwa,” amesema Wakili Shehzad.

Wakili huyo ameongeza kueleza kwamba “Baada ya uchunguzi ikaonekana sina hatia na huruma ya DPP nilikuwa nafaa kuwa shahidi ndio nikaachiwa huru, Meneja alikiri kosa akalipa faini,”.

Akielezea maisha ya gerezani Shehzad amesema kisaikolojia unakuwa na maumivu makubwa, “Kisaikolojia unaumia sana unaamka una lala unafikiria lini utatoka, kila baada ya siku 14 unajikumbusha kosa lako ni nini na kesi yako ni nini, kuna watu maisha yao yanasimama kwa sababu hawana pesa,” amesema Wakili Shehzad.