Jumatatu , 20th Mar , 2023

Wananchi wanaoishi pembezoni mwa bonde la mto Msimbazi wanaotakiwa kupisha mradi wa uendelezaji wa bonde hilo wameandika barua ya wazi kwa Rais wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kumuomba kuingilia kati zoezi la uthaminishaji

Wanadai kuwa zoezi hilo linafanyika kinyume na makubaliano ya awali

Awali makubaliano yalijengwa katika msingi wa kulipana mali kwa mali tofauti na zoezi linavyofanyika sasa hivyo kumuomba Rais Dkt Samia kuingilia mchakato huo

Mradi wa uendelezaji wa bonde hilo unatekelezwa kupitia benki ya dunia