![](http://eatv.tv/sites/default/files/styles/detailpageimg/public/news/2025/02/18/nyu.jpg?itok=Fu66OA6B×tamp=1739887999)
Nyumba za kupanga (Dar es Saalam)
Watu wengi wanategemea nyumba za kupanga hasa wale ambao ndio wanaanza maisha ya kujitegemea hata ambao tayari wamekwisha fanikiwa pia wengine bado wapo kwenye nyumba za kupanga
Moja ya mkazi mpangaji wa muda mrefu amefichua namna ambayo wenye nyumba hao huwazuia wapangaji wao kuondoka kwa kutumia nguvu za giza na kuwageuza mitaji yao.
“Kwenye nyumba za kupanga unaweza kuishi hata miaka 10, huoni maendeleo yoyote hujaweza kununua hata kijiko. Mwenye nyumba ameshakuona wewe ni mtaji na amekuzuia kuondoka bila wewe kujua"
Ni kweli nyumba za kupanga ni muhimu sana ila mpangaji anapaswa kuwa na malengo ambayo atayatimiza baada ya kipindi fulani.