Ijumaa , 30th Sep , 2016

Jaji wa Shindano la Dance100% 2016 Super Nyamwela amesema anajivunia kuona kwamba vipaji ambavyo vimepatikana katika shindano la Dance100% mwaka huu ni vikubwa ambavyo vinaweza kuisaidia jamii katika mambo mengi.

Super Nyamwela

Nyamwela ameyasema hayo alipokuwa akitoa tathmini yake kuhusu shindano hilo ambalo limemalizika hivi karibuni Jijini Dar es salaam.

“Ukweli makundi mwaka huu yamejitahidi sana kufanya mambo makubwa ambapo kila kundi limeweza kujitiuma na kuonesha kwamba ndani ya jamii kuna vipaji vingi ambavyo vikipata nafasi ya kuonekana vinaweza kufanya vizuri katika jamii na kuendeleza sanaa ya uchezaji nchini” Amesema Nyamwela.

Kwa upande wake Jaji Khalila amesema muamko mdogo wa wadada katika shindano hilo utaimarika zaidi mwaka kesho kutokana na binti pekee aliyefika hatua ya fainali Kibibi kuonesha uwezo wa hali ya juu na kuonesha kwamba wadada wakijituma wanaweza kufika mbali katika sanaa ya uchezaji.

Fainali ya shindano la Dance100% ambalo limemalizika hivi karibuni itaoneshwa na EATV siku ya Jumapili hii saa moja usiku.

Tags: