Ijumaa , 16th Dec , 2016

Msanii  wa bongo movie Lulu ambaye alipata nafasi ya kutoa tuzo ya  muigizaji bora wa kike kwenye tuzo za EATV ya mwaka huu amesema hakuweza kushiriki katika tuzo hizo kwa kuwa 2016 haukuwa mwaka wake wa kazi na kwamba alikuwa ametingwa na masomo.

Lulu

 

Hata hivyo Lulu amesema kwa mwakani 2017 atakuwa nje ya masomo  hivyo mashabiki zake wategemee kazi nyingi zaidi kutoka kwake na vitu mbalimbali ili kuweza kuwaridhisha mashabiki zake ambao walimkosa kwa muda wa mwaka mzima akiwa masomoni.

Pia Lulu hakusita kutoa pongezi kwa waandaaji wa EATV AWARD mwaka 2016 kwa kuandaa tuzo hizo lakini pia kwa kumpa nafasi ya kuweza kutoa tuzo ya muigizaji bora wa kike. 

Tags: