Ijumaa , 22nd Jan , 2016

Serikali imewataka wakandarasi wanaejenga barabara za Mangaka-Mtambaswala yenye urefu wa Kilometa 65.5 na Mangaka-Nakapanya ambayo ina urefu wa kilometa 70.5, kukabidhi barabara hizo kwa wakati uliopangwa.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (Wa kwanza kulia) akipokea taarifa ya Ujenzi wa barabara ya Mangaka –Nakapanya.

Akizungumza katika ziara ya kikazi katika ofisi ya Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa Mtwara, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa, amesema serikali imegundua kuwa wakandarasi hao hawawezi kumaliza ujenzi huo kwa wakati kutokana na kushindwa kujipanga vizuri.

Amesema mkandarasi anaejenga barabara ya Mangaka-Nakapanya, anatakiwa kukabidhi barabara hiyo ifikapo mwezi Juni mwaka huu ikiwa katika ubora unaotakiwa.